Samia aenda Dubai kuwapigania wanawake

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameondoka nchini kuelekea Dubai ambako atahudhuria mkutano wa Jopo kuu la Katibu Mkuu la Umoja wa Mataifa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.

Mkutano huo ujadili masuala mbalimbali ya wanawake duniani na kuandaa ripoti ambayo baadaye itawasilishwa katika Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani mwezi Marchi mwaka huu mjini New York, Marekani.

Katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameagwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.