JIFUNZE MBINU MBALIMBALI ZA UJASIRIAMALI ILI UFANIKIWE


Katika ulimwengu wa sasa ambao ajira zimekuwa ngumu na shida kupatikana, ujasiriamali na biashara vimekuwa ndio kimbilio la wengi. Watu wengi wanaingia kwenye biashara kama njia kuu ya kujipatia kipato.
Pamoja na biashara kuonekana kuwa kimbilio la wengi sio wote wanaoingia kwenye biashara wanafanikiwa. Tafiti zinaonesha kwamba asilimia tisini ya biashara zinazoanzishwa zinakufa mwaka mmoja baada ya kuanzishwa. Na hata hizo zinazovuka mwaka mmoja asilimia tisini hufa baada ya miaka mitano. Hivyo kama mwaka huu zimeanzishwa biashara mia moja basi miaka mitano ijayo ni biashara moja tu itakayokuwa bado inadumu.
Kwa nini biashara nyingi zinashindwa kudumu?
Biashara nyingi zinakufa kutokana na ukosefu wa elimu muhimu kuhusiana na biashara na ujasiriamali. Watu wengi wanaoingia kwenye biashara wanaingia kwa kuangalia tu ni kitu gani watu wengine wanafanya na wao kufanya hivyo hivyo.
Biashara ni rahisi sana kufanya ila ni ngumu kuendesha na kuikuza mpaka iweze kukupa faida kubwa sana. Ili uweze kuendesha na kukuza biashara itakayokupa faida kubwa ni muhimu kuchukua muda na kujifunza vitu vya muhimu vinavyohusiana na biashara.
Ungana na mimi katika mfululizo wa masomo ya Ujasiriamali.
                              UJASIRIAMALI NI NINI?

Ujasiriamali ni uwezo wa mtu kuona, kugundua, kuvumbua fursa mbali mbali za kiuchumi na kuziongezea ubunifu ama thamani kwa kuziwekea utofauti kisha kuthubutu na kuzifanya fursa kwa lengo la kutengeneza faida/kipato.
a)      uwezo wa kugundua, kuona na vumbua
b)      fursa za kiuchumi (kilimo, elimu, biashara, utamaduni)
c)      kuziongezea thamani kwa kuongeza ubunifu (ubunifu ktk vionjoo, ufungashaji, masoko)
d)       uthubutu wa kufanya kwa tahadhari (kuanza na mtaji/uzalishaji mdogo ukilenga wateja wengi)
e)      Tengeneza faida kubwa (maximize profit)
MWANZO WA UJASIRIAMALI:
1)      Wazo mahususi(specific idea).Linalo kidhi mahitaji ya jamii(linatatua matatizo ya jamii)
2)      Utafiti (ukubwa wa soko na bei“market share”, tabia za wateja, kipato cha wateja namna ya uzalishaji, gharama za uzalishaji, washindani, sehemu ya biashara   “location”)
3)      Malengo na Mipango (plan) (jinsi ya kuzalisha, wakati, mahali, kupata soko, kupanga bei, kukuza mradi)
4)      Mchanganuo ni taarifa zote zinazo hususiana na mradi zinaweza kuwa nzuri au mbaya).
5)      Mtaji (watu, fedha, ujuzi, umaarufu)
6)      Weka ubunifu (innovation) utofauti (katika) masoko, wazo, ufungashaji, wakati wa uzalishaji).
7)      Mwanzo wa mradi.
SIFA ZA MRADI WA KIJASIRIAMALI.
A)    Ni endelevu kwa kuwa na mipango na mfumo wa utawala ulio wazi (anakufa mmiliki na si mradi).
B)     Unatatua matatizo / changamoto za jamii.
C)    Unatumia rasirimali chache (watu, mtaji, ardhi,muda) na una faida kubwa kwa mapema au mara kwa mara.
D)    Unasoko kubwa  na ushindani mdogo kutokana na ubunifu, wakati wa uzalishaji au sehemu)
MJASIRIAMALI MZURI (mambo ya kuzingatia)
1)      Elimu rasmi na siyo rasmi juu ya mradi.
2)      Ujuzi wa mambo utumiaji wa elimu uliyoipata ama uliyo nayo.
3)      Huruka ya kupata mafanikio halali. (uthubutu, ubunifu, mvumilivu na jasiri, wepesi wa kuona au kuiga, jitahidi kufanya kazi kwa faida jituma)
4)      kujiwekea malengo kila hatua, anashaurika na anabeba majukumu,
5)      Nidhamu ya kazi, fedha, rasirimali, kuipenda kazi yake.
6)      Hakimbii changamoto.
7)      Anatunza kumbu kumbu
8)      Kupata taarifa za mradi kila inapo bidi na kufanya tathimini.
9)      Amechochewa au mwenye vichocheo vya kuendelea kiuchumi kwa kutafuta njia mpya za kujikwamua au kufanya jambo.
MISINGI YA UJASIRIAMALI.
1)      Elimu ya ujasiriamali na kujifunza. Kujifunza mambo tofauti ya miradi yake.
2)      Ubunifu na uvumbuzi. Kuingiza bidhaa mpya katika soko na zinazo kidhi matakwa ya jamii.
3)      Kukua na kupanuka. Kuwa na mipango ya kuendeleza au kukuza biashara yake kiutawala, bidhaa, huduma au uzalishaji.
4)      Kujaribu na kudhamiria. Si mwoga wa kutumia fursa anayo iona.
Kabla ya kuanzisha mradi au kubuni wazo la biashara unapashwa kujiandaa kiakili na hisia kuzifuata ndoto zako na kuifanya kazi utakayo ipenda, kujivunia na kuweza kuizungumzia mbele ya jamii.
       MAONO (VISION) Nini? matarajio yako baada ya kutekeleza wazo/mradi wako (future plan).
   (MISSION) SABABU-ya kufanya mradi huo na si mingine (statement of purpose) lazima ionyeshe kutatua tatizo au kutumia fursa iliyopo.
   
MALENGO- ni mambo unayotaka kuyafikia au kuyapata pia unaweza kuweka na wakati.
  
MFUMO WA MALENGO.
1) Mahususi (specific) 
2) Yanapimika (measurable)                                                                    
3) Yanafikika na changamoto (attainable and challangable)
3) Uhalisia (realistic)                         
4) Muda maalumu (time fram)
ITAENDELEA...

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.