BWENI UDSM LAFUNGWA KWA UCHAKAVU:


Bweni la wanafunzi maarufu kama Hall Two katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 396, limefungwa kutokana na uchakavu kupita  kiasi, huku Hall Five linaloendelea kutumika likiwa katika hali mbaya.

Uongozi wa Chuo hicho umesema ukarabati wa mabweni hayo unahitaji sh bilioni 5.5, huku Hall Two pekee likihitaji sh bilioni 2.7.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Utawala), Profesa David Mfinanga, amesema “Tulilazimika kulifungia Hall Two baada ya kuona limechakaa kupita kiwango na huenda likaleta madhara kwa wanafunzi. Tunasubiri fedha zitakapopatikana tulifanyie ukarabati”.

Kutokana na hali hiyo, Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii imeitaka serikali kuangalia upya suala la kuelekeza taasisi zake kupeleka mapato yake yote hazina, kwani inachangia kukwamisha kwa shughuli zinazohitaji fedha.

Na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Serukamba, amesema Serikali ingekuwa inaacha sehemu ya mapato yanayokusanywa kwenye taasisi husika, yangesaidia mambo kadhaa ikiwamo ukarabati wa miundombinu na iwapo ukarabati ungefanyika mapema kusingekuwa na sababu ya kufungwa bweni hilo, ilhali kuna uhaba wa malazi kwa wanafunzi.

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.