Mkulima mwingine apigwa sime Kilosa
Mkulima mwingine apigwa sime Kilosa
Mkulima aliyefahamika kwa jina la Rajabu Ayoub anayetoka kijiji cha Mbigiri wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro amekatwa na sime akiwa shambani kwake na kumsababishia maumivu makali.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba akizungumza na makundi ya wakulima na wafugaji mkoani Morogoro.
Tukio hilo limetokea baada ya agizo la Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba kuviagiza vyombo vya ulinzi na Usalama kuwashughulikia ipasavyo watakaosababisha kukatwa kwa binadamu au mifugo na kusababisha vifo kukamatwa na sheria kuchukua mkondo wake.
Tukio hilo limetokea siku chache baada ya mkulima mwingine kupigwa mkuki mdomoni katika wilaya hiyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema mkulima huyo amekatwa na sime maeneo ya kichwani na watu jamii ya wafugaji wakati akijaribu kuwazuia ng'ombe kuingia shambani kwake.
Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye amepata taarifa ya tukio hilo wakati akiendelea na ziara yake mkoani Morogoro ameagiza nguvu ya dola iongezwe kutoka katika jeshi la polisi ili kukamatwa kwa wahalifu hao na kudhibiti vurugu hizo zinazoendelea.
No comments