Kigwangalla atoa sababu wasomi kufeli maisha

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla amefunguka na kuweka bayana sababu ambazo zinawakwamisha wasomi wengi kuingia katika biashara au kazi zisizo rasmi

Amesema uoga wa kujaribu kuwa ndiyo kikwazo kikubwa kwa wasomi wengi wa Tanzania.
Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema hayo kupitia ukurasa wake wa twitter na kusema mfumo wa elimu ya Tanzania ndiyo chanzo kikuuu kwa wasomi wengi kuwa waoga kwani wanajengwa katika misingi ya ubinafsi kupitia mitihani.

"Uoga wa kujaribu umewajaa wasomi, hawako tayari kuchukua 'risk' ama kufanya kazi zisizo rasmi. Hiki ni kikwazo kikubwa cha maendeleo. Wengine wanasema 'mentality' ya ubinafsi tunaitoa kwenye mfumo wa elimu wa kufanya mitihani binafsi, wakati mtaani panahitaji ushirikiano. Msingi wa wasomi kutofanikiwa kujiajiri ni mfumo wa elimu unaojenga ubinafsi na kuminya ubunifu na uhuru wa fikra" alisema Dkt. Kigwangallah

Mbali na hilo Dkt. Hamisi Kigwangalla alitoa maoni yake na kuwataka watu wapunguze mifumo ya ubinafsi ili mwisho wa siku watu waweze kuwa na ujasiri wa kufanya maamuzi na kuingia katika vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kuleta tija katika maisha yao na kuleta maendeleo kwa taifa.

"Tupunguze mifumo ya ubinafsi, ukaririshaji mashuleni ili kujenga kizazi kipya cha wabunifu, wajasiri na wenye uthubutu wa mawazo mapya" aliandika Dkt. Hamisi Kigwangalla

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.