Sanchez ahusishwa na Juventus

Gazeti maarufu la michezo nchini Italia la Tutto Sport limeandika kuhusu mpango wa Juventus kwa Sanchez.Katika mpango huo wa Juventus wanataka kufanya usajili huo kwa kuwapa Miralem Pjanic.

Sanchez ambae mkataba wake umebakiza miezi michache kuisha amekuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka Arsenal.Tetesi za yeye kuondoka Gunnerz zinazidi kusambaa baada ya Sanchez kugoma kusaini mkataba mpya wa kukipiga Guners hadi hapo watakapomuongezea mkataba.

Timu nyingi ikiwemo PSG pamoja na timu za China zimekuwa zikipigana vikumbo kuhusiana na saini ya mchezaji huyo.Lakini sasa Juventus nao wameingia kwenye mbio hizo.Taarifa zilizotolewa na gazeti la Tuttos zinasema Juventus wanataka kumuweka Miralem Pjanic kuwa sehemu ya dili hilo.

Sanchez anaonekana uhusiano wake na Wenger unazidi kuporomoka kwani wikiendi hii alionekana mwenye hasira kubwa bada ya kutolewa katika mchezo zidi ya Swansea.Sanchez anataka Arsenal wamuongezee mkataba awe analipwa £280,000 kwa wiki jambo ambalo linaonekana gumu.

Juventus baada ya kufanya usajili wa rekodi Italia kwa kumchukua Higuain kwa dau la £76m akitokea Napoli.Baada ya kumuuza Paul Pogba Juventus wanaonekana kuxidi kutaka kuitengeneza timu yao na kumtafuta mtu wa kucheza pamoja na Paulo Dyabala na Gonzalo Higuain,Sanchez anaonekana mtu sahihi kwao kwa sasa.



No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.