Aboutrika atajwa kwenye listi ya magaidi huko Misri


Mamlaka za usalama za Egypt zimemweka mchezaji wa zamani wa soka wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Mohamed Aboutrika katika ya magaidi baada ya kuhusishwa na kikundi cha waislam wa Brotherhood, amesema mwanasheria wa mchezaji huyo.
 

Mr Aboutrika anashutumiwa kuwasaidia kifedha kikundi cha  Brotherhood, kikundi ambacho mamlaka za Misri kimewaeka kwenye kundi la magaidi.


Mnamo mwaka 2012, alimpigia kampeni ya urais Mohamed Morsi, ambaye ni mwanachama wa Brotherhood.

Jambo hilo lilipelekea kuwagawa mashabiki wa mchezaji bora wa mwaka wa BBC wa mwaka 2008. 

Kwa sheria za Misri, mtu yoyote anayewekwa kwenye listi ya ugaidi, hufungiwa kusafiri na passport yake pamoja na mali zake hushikiliwa. 

Mwanasheria wa Aboutrika, Mohamed Osman, alisema mteja wake hajatiwa hatiani wala hajapewa taarifa rasmi juu ya mashtaka wanayomtuhumi nayo. Pia ameahidi kukata rufaa juu ya tuhuma hizo kwa mteja wake. 


Kiungo huyo wa zamani wa Al-Ahly na timu ya taifa ya Misri, alikuwa kipenzi cha wananchi wa Misri na walifikia hatua ya kumpa  majina ya  The Prince of Hearts, The Magician na The Saint wakati akicheza soka, lakini uamuzi wake wa kumsapoti Mohammed Morsi, ambaye alikaa madarakani kwa mwaka mmoja tu, uliwagawa mashabiki zake. 

Mwaka 2015, mali zake nyingi ziliwekwa kizuiani, hisa zake kwenye makampuni tofauti zilishikiliwa na mamlaka za usalama za nchi hiyo. 

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.