Picha za uwanja mpya wacTottenham Hotspur zatolewa

Klabu ya Tottenham Hotspur ya Uingereza imetoa picha za kwanza za uwanja wa klabu hiyo ambao unaendelea kujengwa kaskazini mwa London.

Uwanja huo, ambao utatoshea mashabiki 61,000, utakuwa ndio mkubwa zaidi wa soka katika jiji kuu la London utakapofunguliwa mwaka 2018.

Miongoni mwa mengine, utakuwa na baa kubwa zaidi ya kuhudumia watu wote uwanjani Uingereza. Aidha, viti vyake vitakuwa na mitambo ya kubadili viwango vya joto.

Kutakuwa pia na kiwanda kidogo cha kutengeneza pombe na pia kiwanda kidogo cha kuoka mikate na keki.

Mwenyekiti wa Spurs amesema uwanja huo utaleta "taswira mpya kwa michezo na burudani".

Uwanja huo utakuwa na sakafu iliyopandwa nyasi ambayo inaweza kuondolewa na chini yake kutokee sakafu ya mkeka.

Hilo litawezesha uwanja huo kuwa mwenyeji wa mechi za kandanda, NFL, matamasha pamoja na hafla nyingine.

Muonekano wa uwanja huo kwasasa
Miongoni mwa mengine, uwanja huo utakuwa na:

Njia iliyozingirwa kwa kioo cha kutumiwa na wachezaji kuingia uwanjani. Hii itawawezesha mashabiki kutazama yanayojiri kabla ya mechi.

Eneo la kuuzia bia la umbali wa 285ft (86.8m) ambapo kila mtu atauziwa

Mfumo mpya wa kusambaza bia ambao utawawezesha wauzaji kutoa painti 10,000 za bia kila dakika.

Viti vitakuwa na mitambo ya kuongeza joto na sehemu za kuwezesha mtu kutumia vifaa vya USB.

Kutakuwa na sehemu moja ya kuketi watu 17,000, ambayo itakuwa kubwa zaidi Uingereza.

Ujenzi wa uwanja huo utagharimu £750m lakini utabuni nafasi 3,500 za ajira eneo hilo utakapokamilishwa, kwa mujibu wa klabu hiyo.

Watu kwenye mgahawa wa orofa ya tisa wa Sky Lounge wataweza kutazama vizuri yanayojiri

Watu wataweza kuwatazama wachezaji wakiingia na kutoka uwanjani kupitia kioo

 

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.