Neymar aongoza listi ya wachezaji wenye thamani
Paul Pogba ndio mchezaji anaeshikilia rekodi ya Dunia katika gharama za usajili.Pogba alinunuliwa na Manchester United msimu uliopita akitokea Juventus kwa ada ya £89 akivunja rekodi ya Gareth Bale aliyeenda Real Madrid akitokea Totenham Hotspur.
Shirika la CES Football Obsevartory limefanya utafiti wa wanasoka.Utafiti huo ulilenga kutaka kujua thamani ya mchezaji.Katika tafiti hiyo walizingatia kiwango cha mchezaji,umri wake,anavyozungumziwa duniani,umaarufu wake,mkataba alionao na jinsi anavyotajwa tajwa katika tetesi za usajili.Utafiti huu huafanywa kula mwaka na orodha hutolewa January.
Katika utafiti huo inaonekana mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Barcelona Neymar ndiye mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi duniani kwa sasa.Neymar kwa sasa inakadiriwa thamani yake kama ukimtaka ni kati ya £217 – £218m.Thamani hii inatokana na umuhimu wake katika timu ya taifa pamoja na klabu yake,sii hivyo tu ila pia umri wa Neymar ni mdogo akiwa na miaka 24.Japokuwa amecheza dakika 1000 bila goli ila ametoa assist 15 kwenye mechi 21.
Baada ya Neymar anayemfuatia ni pacha mwenzake wa Barcelona Lioneil Messi.Messi thamani yake imeshuka.Mwaka jana katika listi kama hii Messi aliongoza lakini mwaka huu anaonekana thamani inashuka kadri miaka inavyokwenda.Kupoteza Ballon D’or,kutocheza fainali ya UEFA ni moja kati ya vitu vinaonekana kuanza kushisha thamani ya Lioneil Messi.
Paul Pogba yupo nafasi ya tatu pamoja na kwamba Pogba ndiye anaeshikilia rekodi ya usajili wa pesa nyingi lakini ndiye mchezaji wa tatu kwa thamani.Inawezekana Pogba hana thamani kubwa kama Neymar kwa kuwa yeye misimu aliyocheza kwa kiwango cha juu ni michache kuliko ya Neymar bali pia timu anayochezea haipo katika mashindano makubwa ya UEFA hiyo inamshusha thamani.Pengine Manchester United wakishiriki UEFA na thamani yake itapanda.
Antoine Griezman yuko nafasi ya nne baada ya Pogba.Alikuwa na msimu mzuri sana uliopita japo hakufanikiwa kubeba UEFA lakini aliisaidia Athletico na Ufaransa kufika fainali za Ulaya.Nje ya uwanja Griezman ni mtu mpole sana asiye na mambo mengi.thamani ya Griezman kwa sasa ni £132.2m
Luis Suarez anaifunga list ya tano bora.Ambayo tano bora imetawaliwa na La Liga huku mchezaji pekee kutoka nje ya La Liga ni Paul Pogba ansecheza Epl.Uwezo wa Suarez uliisaidia Barca kubeba La Liga,muunganiko wake na Neymar na Messi ni kati ya utatu wakuogopwa sana duniani,Suarez ana thamani ya £127.7m.
Hiyo ndio tano bora ya wachezaji wenye thamani kubwa Duniani.Najua mshangao wa wengi hapo watauliza Cr7 yuko wapi?thamani ya mchezaji inashuka kutokana na umri.Cristiano sasa anaelekea kumaliza soka lake ana miaka 31,ni ngumu timu kutoa hela kubwa kwa mchezaji mwenye umri mkubwa kama wake lakini yupo nafasi ya saba akiwa na thamani ya £111.2m.
Huku Cristiano akiwa nafasi ya saba juu yake ya sita yupo Harry Kane akiwa na thamani ya
£122.4m,na kwa mara ya kwanza Totenham Hotspur wanaingiza wachezaji wawili kwenye listi hii Delle Ali yuko nafasi ya tisa na thamani ya £97m.Ifuatayo ni orodha ya wachezaji 20 wanaotajwa kuwa na thamani kubwa duniani kwa sasa.
1.Neymar (Barceloma) £217m
2.Lioneil Messi (Barcelona) £150m
3.Paul Pogba (Manchester United) £136m
4.Antoine Griezman (Athletico Madrid) £132.2m
5.Luis Suarez (Barcelona) £127m
6.Harry Kane (Totenham) £122.4m
7.Cristiano Ronaldo (Real Madrid) £111.2m
8.Paulo Dyabala (Juventus) £100m
9.Delle Ali (Totenham) £97m
10.Eden Hazard (Chelsea) £89m
11.Gonzalo Higuain (Juventus) £86.6m
12.Anthony Martial (Manchester United) £81.3m
13.Raheem Sterling (Man City) £75m
14.Gareth Bale (Real Madrud) £73m
15.Yannick Carrasco (Athletico Madrid) £73m
16.Sergio Aguero (Man City) £70m
17.Riyad Mahrez (Leicester City) £68.7m
18.Mauro Icardi (Inter Millan) £68.3m
19.Kelvin De Bruyne (Man City) £67.5m
20.Alexis Sanchez (Arsenal) £67.1m
No comments