Jammeh atangaza hali ya tahadhari ya siku 90 nchini Gambia

Rais wa Gambia Yahya Jammeh ametangaza hali ya tahadhari ya siku 90, siku moja kabla ya muhula wake kukamilika rasmi, kwa mujibu wa televisheni ya nchi hiyo.

Viongozi wa kikanda wamekuwa wakimshawishi bwana Jammeh wakimtaka asalimishe madaraka kwa Adama Barrow, ambaye alimshinda kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba.

Hatua hiyo inakuja baada ya Nigeria kutuma meli ya kijeshi kama njia ya kumshinikiza zaidi Bwana Jammeh.

Muungano wa mataifa ya magharibi mwa Afrika ECOWAS, umejiandaa kutumia nguvu, lakini umesema kuwa hatua za kijeshi ndizo zitakuwa za mwisho.

Bwana Barrow anatarajiwa kuapishwa kama rais mpya siku ya Alhamisi

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.