Al-Shabab washambulia kambi ya majeshi ya Kenya nchini Somalia
HakiAFPImageal-Shabab wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa
Kundi la al-Shabab nchini Somalia limesema wapiganaji wake wameshambulia kambi ya wanajeshi wa Kenya wanaohudumu chini ya kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom)nchini Somalia.
Wapiganaji hao wanadai kuwaua wanajeshi wengi kwenye shambulio hilo katika kambi ya Kulbiyow kusini mwa Somalia karibu na mpaka wa nchi hiyo na Kenya.
"Mujahideen (wapiganaji) wawili walivurumisha magari yaliyokuwa na mabomu na kuyalipua kwenye lango la kambi hiyo ya mji wa Kulbiyow kabla ya wapiganaji wengine kuingia. Baada ya makabiliano makali, tumefanikiwa kuiteka kambi," mmoja wa wasemaji wa al-Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab ameambia shirika la habari la Reuters.
Msemaji huyo amedai kundi hilo limewaua wanajeshi zaidi ya 50 na kutwaa magari na silaha za wanajeshi hao, taarifa ambazo msemaji wa majeshi ya Kenya amekanusha.
Kanali Paul Njuguna ameambia Reuters: "Ni uongo. Operesheni ya kijeshi inaendelea.
Al-Shabab wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi na jamii ya kimataifa.
Wanajeshi wa Kenya pamoja na wanajeshi kutoka Djibouti, Uganda na Ethiopia, chini ya Amisom, wamekuwa wakisaidia serikali hiyo yenye makao yake Mogadishu.
Januari mwaka uliopita, wapiganaji wa al-Shabab walishambulia kambi ya majeshi ya Kenya el-Adde na kuua wanajeshi wengi.
Al-Shabab walisema waliua zaidi ya wanajeshi 100. Jeshi la Kenya halijatangaza idadi kamili ya wanajeshi waliouawa hadi wa leo.
No comments