SOMO LA UJASIRIAMALI-SEHEMU YA PILI


NJIA ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA.
A)    Tumia ujuzi ulionao. Mf, fundi magari anaanzisha gereji yake.
B)     Nini kinakosekana mtaani kwako? Kitu kinacho leta usumbufu (haba,hafifu) na kinakuletea kupoteza muda au wakati mwingi. Huduma zipi hazipo mtaani kwako na muhimu? Ni kitu gani,wewe, ndugu,majirani huwa wanakilalamikia sana mtaani kwako?
C)    Tumia mabadiliko ya Technologia. M-pesa, online service.
D)    Uwepo wa taasisi kubwa au matukio (shule, hospitali, ujenzi, harusi)
E)     Kuwa wakala wa bidhaa.
F)     Nakili ubunifu wa watu wengine toka sehemu nyingine.
G)    Nunua biashara iliyopo.
H)    Tumia kipaji chako (ngoma za asili, mziki)


MISINGI MUHIMU MITANO YA BIASHARA
misingi mitano muhimu ya biashara ambayo kila biashara inatakiwa kuizingatia.
Wewe kama mjasiriamali una jukumu la kujifunza na kufuata misingi hii ili uweze kufikia malengo yako kwenye ujasiriamali na biashara.
Misingi mitano muhimu ya biashara.
Ili biashara yoyote iweze kudumu na kukua inahitaji kufuata misingi ifuatayo.
Kutengeneza thamani.
Ili biashara iweze kukua na kutengeneza faida ni lazima itengeneze bidhaa au huduma ambayo ni ya thamani kwa wateja. Ni lazima utoe bidhaa au huduma ambayo watu wanaihitaji sana ili kuboresha maisha yao. Kama hujaanza biashara fikiria ni kitu gani cha thamani ambacho watu wanakihitaji ila wanakikosa, kisha anza kuwapatia na utajenga biashara kubwa. Kama tayari unafanya biashara angalia ni kitu gani cha thamani unachotoa kwa watu na angalia jinsi unavyoweza kuboresha ili kupata wateja wengi zaidi.
Soko.
Kuwa na kitu chenye thamani pekee bado haikutoshi kutengeneza biashara kubwa, ni lazima kuwe na soko linalohitaji bidhaa au huduma hiyo. Hata kama soko lipo bado sio rahisi kwa kila mtu kujua kwamba unatoa huduma muhimu. Hivyo ni muhimu kutafuta soko la biashara yako kwa njia mbalimbali zikiwemo matangazo. Inakubidi uhakikishe watu wanajua uwepo wa biashara yako na utengeneze uteja ili watu waje kupata thamani unayotoa. Kukosa soko la uhakika ni chanzo cha kufa kwa biashara nyingi.
Kuuza.
Ili biashara ikue ni lazima uweze kuuza thamani uliyotengeneza. Ni muhimu uweze kuwashawishi watu wanunue bidhaa au huduma unayotoa. Kuuza ndio moyo wa biashara ambapo kama usipokuwa makini ni rahisi kwa biashara kufa.
Kufikisha thamani.
Kama umewaahidi wateja wako kwamba bidhaa ama huduma unayotoa itaboresha maisha yao basi hakikisha hicho ndio kitu kitakachotokea kwa wateja. Ni lazima uweze kufikisha thamani uliyoahidi kwa wateja. Kwa kushindwa kufanya hivi wateja watakuona wewe ni tapeli na hawatanunua tena bidhaa yako. Kama biashara itashindwa kutengeneza wateja wanaojirudia ni lazima itakufa.
Fedha.
Usimamizi wa fedha ni muhimu sana kwenye biashara. Ili biashara iweze kudumu ni lazima iweze kutengeneza mapato makubwa kuliko matumizi na uzalishaji. Ni lazima iweze kuzalisha fedha za kutosha kuiendesha na ibaki faida. Ukosefu wa fedha unaotokana na mauzo kidogo na matumizi makubwa ndio chanzo cha kufa kwa biashara nyingi.
Misingi hii mitano ni muhimu sana kwa biashara. Hakuna msingi ambao unaweza kusema ni muhimu zaidi ya mwingine, yote inategemeana. Ili biashara yoyote iweze kudumu ni muhimu kuzingatia misingi hiyo.
ITAENDELEA....
For Adverts:
mwasebainfo@gmail.com

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.