Makardinali Wapanga Kumshinikiza Papa Ajiuzulu..!!!


Jopo la Makardinali waliompa ushirikiano mkubwa Papa Francis wa 16 wakati wa uteuzi wake, wamepanga kumshinikiza ajiuzulu kutokana na ukiukwaji wa maadili ya kanisa.

Gazeti la The Times na Libero la Italia, yameandika kuwa Makardinali hao zaidi ya dazeni, wamepanga kushinikiza Papa Francis ajiuzulu lakini bila kujitenga naye kwa namna yoyote ile. Hata hivyo haijafafanuliwa ni maadili gani aliyoyavunja Papa huyo.

Makardinali hao ndiyo waliofanya jitihada kubwa za kuteuliwa kwa Papa Francis katika uteuzi wa nafasi hiyo mwaka 2013.

Mwandishi  Antonio Socci ameandika katika gazeti la Libero na kueleza kuwa kwa sasa  Makardinali wanajadili iwapo Papa akijiuzulu nani atashika nafasi yake.

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.