WAMTAKA OBAMA KUGOMBEA URAIS UFARANSA


WAMTAKA OBAMA KUGOMBEA URAIS NCHINI UFARANSA

Ufaransa inatarajia kufanya uchaguzi wa Rais mwezi Aprili mwaka huu ambapo wagombea kadhaa wamejitokeza.

Hata hivyo katika hali ambayo isiyotarajiwa na wengi, wananchi ambao hawaridhiki na wagombea waliojitokeza wameanza harakati za kufungua mashtaka ili kuitaka Mahakama Kuu ya nchi hiyo kutoa kibali cha Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama kugombea nafasi hiyo.

Kampeni hiyo iliyopewa jina la OBAMA17 inaenda sambamba na kutafuta saini za waungaji mkono 1,000,000 wa azimio hilo litakaloruhusu mashauri ya raia asiye raia wa Ufaransa kugombea nafasi ya Rais wa nchi hiyo kuweza kusikilizwa. Hadi jana zaidi ya watu 500,000 walikuwa wamesaini kuunga mikono azimio hilo.

Maeneo mbalimbali nchini ufaransa yamepambwa na mabango  yanayohamasisha mpango huo yenye kauli mbiu isemayo 'Oui on peut', ikimaanisha 'Yes we can'.

Wafaransa wanaounga mkono azimio hilo wanasema Rais mstaafu Barack Obama ana sifa za kuongoza Taifa lolote duniani.

Aidha, wanaotetea hoja hiyo wanasema huu ni wakati wa kutafuta watu wenye uwezo ambapo kigezo cha uraia hakina mantiki kwani kwa miaka migi viongozi raia ndio wamekuwa wanaididimiza Ufaransa.

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.