VIJANA WAJITOLEA UJENZI WA MABWENI YA SHULE




Ujenzi wa KUJITOLEA wa mabweni, vyumba vya madarasa na nyumba za walimu katika shule ya sekondari Nasibugani iliyoko Mkuranga unaendelea.

Baada ya vijana wasomi wa vyuo vikuu zaidi ya 50 kujitolea kufyatua matofari elfu 45 na kisha kikosi cha JKT Ruvu kuanza kujenga majengo kwa kujitolea.

Katika video, inaonyesha namna ujenzi ulivyofikia kiwango cha kuridhisha na inaonyesha ni kwa namna gani vijana hasa wasomi wakatumia nafasi zao mbalimbali kufanya mamva chanya katika ujenzi wa Taifa.
Rai yangu ni Kwa Vijana wote wa Tanzania kuwaambia mabadiliko katika maendeleo ya Taifa hayaletwi na Rais peke yake , hivyo basi kila mmoja kwa nafasi yake anao mchango mkubwa sana katika kuleta mapinduzi ya Maendeleo.

Naomba Serikali iaiwaache hawa vijana mashujaa ambao wameamua kujenga mabweni ya shule ili vijana wenzao wasome katika mazingira mazuri na wao waweze kufika chuo kikuu kama wao, ili iwe chachu kwa vijana wengine.
Hakika huu ni uhodari na ndo vijana wa aina hii wanaotakiwa katika nchi hii ya Tanzania.

Nchi yangu...
Matokeo chanyA

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.