Kesi dhidi ya anayedaiwa kuwa malkia wa tembo yaendelea kuunguruma.
Anayedaiwa kuwa Malkia wa Tembo,Yang Feng Clan anyedaiwa kujihusisha na biashara ya meno ya tembo ya zaidi ya bilioni 13 akirudishwa mahabusu.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa mshtakiwa Salvius Matembo anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kujihusisha na biashara ya Meno ya Tembo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 13.9 alijaribu kuwatoroka polisi walipoenda kumkamata.
Askari wa Jeshi la Polisi Idara ya Upelelezi na Makosa ya Jinai, Koplo Emmanuel John alisema hayo leo wakati akitoa ushahidi wake mbele ya hakimu mkazi, Huruma shahidi kama shahidi wa pili.
Mshtakiwa matembo anashtakiwa pamoja na raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu, Yang Feng Glan (66) na Manase Philemon.
Akiongozwa na wakili wa Serikali, Paul Kadushi, Koplo Emmanuel alidai kuwa Mei 14,2014 akiwa ofisini kwake makao makuu ya polisi akiwa na askari wenzake waliitwa na msaidizi wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Mkosa ya Jinai na kupewa jukumu la kumtafuta Matembo.
Amedai kuwa baada ya siku saba, Mei 21, 2014 ndipo alipofanikiwa kumkamata Matembo baada ya kupata taarifa kutoka kwa msiri wao kuwa mtuhumiwa huyo alionekana katika baa ya Kilimanjaro iliyopo Sinza .
Amesema kuwa, kwa kuwa hakuwa akimfahamu mtuhumiwa alienda na msiri huyo hadi katika baa hiyo na kufanikiwa kumkamata baada ya kuonyeshwa alipokuwa amekaa na kujitambulisha kuwa wao ni polisi na kumueleza yupo chini ya ulinzi kwa kujihusisha na Meno ya Tembo .
Aliongeza kuwa Matembo alitaka kutoroka lakini kwa kuwa walijipanga aliweza kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi.
Alieleza kuwa baada ya hapo walimpeleka katika kituo cha polisi cha Kijitonyama lakini kabla ya kumfikisha, wakiwa njiani Matembo aliwashawishi kuwapa rushwa ili wamuachie lakini walikataa.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22,2014 walijihusisha na biashara ya nyara za serikali.
Katika kipindi hicho washtakiwa hao wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogramu 1889 zenye thamani ya Sh 5.4 bilioni bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyama Pori.
Wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22,2014 kwa makusudi raia wa China, China, Yang Feng Glan aliongoza na kufadhiri vitendo vya kijinai kwa kukusanya na kusafirisha vipande hivyo 706 vya Meno ya Tembo bila ya kuwa na kibali chochote kile kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama Pori.
Kwa upande wa washtakiwa Salvius na Manase wanadaiwa kuongoza makosa ya uhujumu uchumi kwa kusaidia biashara ya nyara za serikali kwa kukusanya, Kusafirisha na Kuuza Meno ya Tembo kwa nia ya kujipatia faida.
Ilidaiwa kuwa Mei 21, 2014 katika eneo la Sinza Palestina wilaya ya Kinondoni mshtakiwa Manase alitoroka chini ya ulinzi halali wa askari wa Jeshi la Polisi D 7847 Koplo Beatus ambaye alikuwa akimshikilia kwa makosa ya kujihusisha na biashara za nyara za serikali.
No comments