Kauli 20 za Kamishna wa Kupambana na Dawa za Kulevya Wakati Akitangaza Vita Mpya.
Kamishna wa kupambana na dawa za kulevya, Rogers William Sianga amelipigilia msumari kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya.
Alikuwa akiongea leo jiji Dar es Salaam katika mkutano ulioandaliwa na mkuu wa Mkoa, Paul Makonda baada ya kukabidhiwa orodha ya tatu ya majina ya watu wanaohusishwa kwenye biashara hiyo.
Kamishna Sianga amesema hawatamuonea huruma mtu yeyote anayejihusisha kwenye biashara hiyo. Ameomba vita hiyo kuendelea nchi nzima na Dar es Saalam peke yake akidai itaendelea hadi visiwani Zanzibar.
Pia amempongeza Paul Makonda kuanzisha mapambano hayo.
Hizi ni baadhi ya nukuu kutoka kwa Kamishna Sianga kutoka kwenye mkutano huo.
1. Sisi waliotukabidhi kazi hii tutaifanya kwa bidii
2. Wauzaji wa dawa za kulevya wanasababisha HIV, kukosa uwezo wa kuzaa, ugonjwa ini na TB
3. Muuzaji wa dawa za kulevya anasabisha watu wasilime chakula, anasabibisha njaa
4. Biashara ya madawa ya kulevya inasababisha ‘inflation’ (kupanda bei kwa bidhaa)
5. Suala la madawa ya kulevya hakuna mtu ambaye yupo salama Atakapotokea muathirika nyumbani kwako ndio utajua madhara yake
6. Tumepokea orodha tuliyopewa na Mkuu wa Mkoa, tempo ni hiyo hiyo
7. Kumekuwepo na mahakimu au majaji wanaovuruga kesi zetu za madawa ya kulevya, tunaanda orodha yao
8. Kumkatisha ghafla mtu aliyeathirika na dawa za kulevya atakufa. Ukimweka jela atapata maumivu makubwa
9. Tutakutana na wamiliki wa sober houses ili kuweka utaratibu wa namna ya kuwasaiia waathirika wa dawa za kulevya
10. Mtu ambaye anafanya biashara ya dawa za kulevya au utakatishaji wa fedha huyo tunakwenda naye
11. Sheria mpya inatupa uwezo wa kukukamata hadi mali ambazo umezichuma kutokana na biashara ya dawa za kulevya
12. Tutakuelezea namna ya kukutoa kwenye dawa za kulevya. Lakini utatuambia nani anayekuuzia hayo madawa
13. Tutaanzaisha kampeni za dawa ya kulevya kuanzia shuleni hadi vyuoni
14. Vita vya dawa ya kulevya sio vya Dar tu. Alichokianzisha Makonda tunataka nchi nzima moto uwake, hatobakia mtu
15. Heroin inaharibu mwili na kisaikolijoa, uraibu wake ni mbaya zaidi
16. Mirungi inamfanya mwanaume asiwe mwanaume, mirungi inaua ndoa
17. Wafanyabiashara wa dawa za kulevya wameleta huzuni nyingi katika familia, hatutokuwa na huruma nao
18. Mtumiaji wa madawa ya kulevya hutesa familia na kuirudisha nyuma
19. Uzuri wa muuza dawa za kulevya anatamba
20. Tutakuwa na kitengo cha kuwasaidia walioathirika na dawa za kulevya
No comments