CWT yapanga kutangaza mgogoro na Serikali

Dar es Salaam.Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimesema kitatangaza mgogoro na Serikali ifikapo Februari 28 mwaka huu ikiwa haitaeleza ni lini italipa madai yao yanayofikia Sh 800 bilioni.

Akizungumza leo, Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha baraza la taifa la chama hicho kilichofanyika mkoani Morogoro.

Amesema kati ya fedha hizo Sh 300 bilioni ni stahili zao za kupandishwa madaraja wakati Sh 480 ni mafao ya walimu wastaafu.

Amesema Serikali imekuwa ikilipa madai ya walimu taratibu kiasi kwamba yanazidi kuongezeka.

"Kwa kuwa Serikali inazidi kulimbikiza madai ya walimu tunaona zipo dalili za kuzidiwa na madeni haya na hivyo kushindwa kuwalipa walimu.”

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.