Wanandugu bungeni wazua mjadala


Dar es Salaam. Inaweza kuonekana kuwa ni kitu cha ajabu kwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo kuingia kwenye Bunge ambalo tayari yumo binti yake Halima, lakini hii si mara ya kwanza kwa wanandugu na wanandoa kuwa ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria kwa wakati mmoja.

Bulembo, kiongozi wa zamani wa soka, ameingia ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli juzi, sambamba na mwanasheria nguli, Profesa Palamagamba Kabudi.

Rais ametumia mamlaka anayopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ibara ya 66(1) kuteua watu kumi kuwa wabunge 10.

Wakati uteuzi wa Profesa Kabudi ukiibua mjadala wa uwezekano wa kuwapo mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri, wa Bulembo umeibua mjadala kutokana na bintiye, Halima Bulembo kuwa mmoja wa wabunge walioteuliwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi.

Halima ameingia bungeni kwa tiketi ya viti maalumu kwa nafasi ambazo Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umetengewa.

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.