Wanafunzi Mtwara waenda Ireland Wanapata ufadhili baada ya kushinda sayansii

Wanafunzi Mtwara waenda Ireland Wanapata ufadhili baada ya kushinda sayansi

Wanafunzi wawili kutoka Shule ya Sekondari ya wasichana MTWARA waliopta ushindi wa jumla kwenye Shindano la Wanasayansi Chipukizi hapa nchini mwaka jana, wanaondoka leo kuelekea Dublin nchini Ireland kwa ajili ya kushuhudia tafiti mbalimbali za kisayansi zilizofanywa na wanafunzi wa nchi hiyo hatua itakayowaongezea ujuzi na uwezo katika masauala ya elimu ya sayansi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Taasisi inayoshughulika na ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Tanzania (KARIMJEE JIVANJEE FOUNDATION) Yusuph Karimjee amesema wanafunzi hao DIANA SOSOKA na NAGRA MRESA wanatarajia kujifunza mambo mbalimbali wakiwa nchini Ireland hususan katika nyanja za sayansi na teknolojia.

Kwa Upande wao wanafunzi hao wameishukuru Taassisi ya Karimjee pamoja na Shirika la Wanasayansi Chipukizi kwa kuthamini elimu ya wanafunzi wa Tanzania na kwamba elimu hiyo wataitumia kama chachu ya kuondoa umasikini ndani ya jamii ya Kitanzania pamoja na kusaidia waishio katika mazingira Magumu..

Wanafunzi hao walioibuka washindi katika Shindano la Wanasayansi Chipukizi lililojumuisha zaidi ya wanafunzi 300 kutoka shule mbalimbali hapa nchini, ambapo mbali ya ziara hiyo pia walipatiwa ufadhili wa masomo ya kuendelea kidato cha tano na sita kutoka Taasisi ya KARIMJEE JIVANJEE FIUNDATION.

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.