Wafungwa wakatwa vichwa ndani ya gereza Brazil

 Polisi wa kukabiliana na ghasia nchini Brazil wanajaribu kila wawezavyo kuingia ndani ya gereza kuu katika jimbo la Rio Grande do Norte, ambalo limetwaliwa na wafungwa.

Idara ya olisi inasema kuwa, zaidi ya wafungwa kumi wameuwawa baadhi yao kwa kukatwa katwa katika makabiliano makali kati ya magenge hasimu katika gereza hilo la Alcaçuz.

Polisi hao wamefika nje ya ukuta wa gereza hilo wakisubiri hadi kutakapopambazuka ndipo waingia ndani.

Mwaka jana pekee zaidi ya wafungwa 100 wamefariki katika makabiliano kama hayo yaliyofanyika awali mwezi huu nchini humo katika magereza yaliyoko katika majimbo ya Amazonas na Roraima.


No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.