Vodacom kutoa hizi bilioni 32 kwa wateja wake

Wakati wateja na wananchi mbalimbali wakiendelea kunufaika na promosheni ya Nogesha Upendo ya Vodacom kwa kujishindia mamilioni ya fedha kila siku pindi wanunuapo vifurushi kwenye simu zao.

vodacom hawajaishia hapo sasa wameileta hii ya malipo ya faida ya kutumia M-Pesa ambayo imeanza wiki hii na inaufanya mwanzo wa mwaka mpya kuwa mzuri zaidi kwa mamilioni ya wateja na mawakala wa M-Pesa.

Unaambiwa awamu hii ya malipo ya faida ya utumiaji wa M-Pesa inafikia jumla ya Tsh Bilioni 32/- ambapo kila mtumiaji atapata sehemu ya gawio kulingana na matumizi ya akaunti yake ya M-Pesa. Malipo haya yatafanyika kwa awamu na yatawanufaisha wateja na mawakala wa M-Pesa waliopo kila kona ya Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa mtandao wa Vodacom kuwarudishia faida ya gawio hilo.

Kampuni ya Vodacom  imekwishagawa zaidi yaTsh Bilioni 39 katika awamu zilizopita na hii inamaanisha kwamba awamu hii itakapokamilika ni zaidi ya Tsh Bilioni 70 zitakuwa zimewekwa moja kwa moja kwenye mifuko ya wateja vodacom.

Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Ian Ferrao amesema ……>>>‘Kila mtumiaji wa M-Pesa atapata pesa ya ziada kwenye akaunti yake ambayo atakuwa na uhuru wa kuitumia vyovyote anavyopenda kama kununua vifurushi, kulipia huduma na bidhaa au kuwatumia ndugu na jamaa zake. Mteja mwenye matumizi makubwa kwenye M-Pesa, anapata gawio kubwa zaidi la faida’

Ukitaka kuona kiasi cha gawio lako, tuma SMS yenye neno KIASI kwenda 15300 na utapokea SMS inayoonesha kiasi cha pesa kitakachotumwa kwenye akaunti yako, vilevile vifurushi vya Cheka, Intaneti, na Ya KwakoTu vinaweza kununuliwa kwa kutumia gawio hili la faida na kununua vifurushi kwa kutumia pesa uliyopokea, Piga 15000# chagua NUNUA MUDA WA MAONGEZI/VIFURUSHI kisha chagua kifurushi unachohitaji.

Promosheni ya Nogesha Upendo ipo kwenye wiki ya 7 sasa ambapo zaidi ya wateja 200 washajishindia Tsh Milioni 1 pesa taslimu  na 600 wengine wameshashinda Tsh 100,000/- za kilasiku. Kuendelea kuongeza nafasi za kushinda zawadi za siku na wiki za hadi TshMilioni 1/- mteja anatakiwa kununua kifurushi chochote cha Vodacom ambapo ataingia kwenye droo moja kwa moja.

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.