UCHUMI WA MIKOA YA KANDA YA ZIWA WAPANDA



Mwanza. Uchumi wa mikoa ya kanda ya ziwa kwa mwaka 2015/16 uliongezeka kwa asilimia 13 na kufikia Sh23.4 trilioni kutoka Sh20.6 trilioni 2014/15.

Ukuaji huo uliochangiwa na Mkoa wa Mwanza kwa asilimia 36.1, umesababisha kuongeza uchumi wa Taifa kwa asilimia 25.7.

Meneja wa Uchumi Mikoa ya Kanda ya Ziwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani Mwanza, James Machemba alisema kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), sekta zilizochangia ukuaji huo ni madini, biashara, utalii na fedha.

Alisema mauzo ya madini nje ya nchi yaliongezeka kwa asilimia 1.4 hivyo kufikia Dola 1,329.5 milioni za Marekani katika mwaka ulioishia Juni 2015/16 kutoka Dola 1,311.3 milioni mwaka 2014/15.

Alisema watu waliotembelea mbuga za wanyama walisaidia kuongeza pato la mikoa ya kanda hiyo kwa asilimia 21.3.

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.