TACAIDS kuwachukulia hatua wanaowapotosha watumiaji wa dawa za VVU.
Tume ya Taifa ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS) kwa kushirikiana na vyombo vya dola inatarajia kuanza operasheni maalumu hivi karibuni ya kuwasaka baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini na waganga wa tiba za asili wanaowapotosha wagonjwa wa ukimwi wanaotumia madawa ya kufubaza virusi vya ugonjwa huo kwa kuwashawishi waache kutumia madawa hayo badala yake waishi kwa imani ya uponyaji wa njia ya miujiza.
Akizungumza na waandishi wa habari,Mwanasheria wa TACAIDS,Elizaberth Mzelu, amesema sheria namba 27 inayohusiana na masuala ya kinga dhidi ya ugonjwa wa ukimwi iliyotungwa mwaka 2008 inamzuia mtu yoyote kujitangaza kuwa anatibu ukimwi au anamkinga mtu asipate virusi vya ukimwi.
Kwa upande wake,Dkt.Subilaga Kaganda Mtaalamu wa afya ya jamii wa TACAIDS amesema serikali ina mkakati mkubwa wa kumaliza tatizo la maambukizi ukimwi ifikapo mwaka 2030 na ameeeleza kuwa mkakati huo kwa sasa unatekelezwa katika hatua mbalimbali.
Naye,Mratibu wa mkoa wa Kagera wa ICAP Dkt.Omary Msumi ameiomba serikali iendelee kutoa elimu juu umuhimu wa matumizi wa dawa za kufubaza virusi vya ukimwi,Charles Mwafimbo afisa ustawi wa jamii mkoani Kagera aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa warsha ya kujadili mpango kazi wa taifa wa kinga ya ukimwi wa kuanzia mwaka 2016-2018 kwa niaba ya Katibu Tawala Kagera Kamishina Diwani Athumani ameagiza kamati za kupambana na ukimwi kuanzia ngazi za vijiji zifufuliwe.
No comments