Mtoto wa miaka 3 amekufa na 16 kujeruhiwa baada ya mvua ya mawe kunyesha Shinyanga.
Mtoto wa miaka 3 amekufa na 16 kujeruhiwa baada ya mvua ya mawe kunyesha Shinyanga.
Mtoto mmoja wa miaka mitatu amepoteza maisha huku nyumba kadhaa zikiwa zimeanguka na kujeruhi watu zaidi ya kumi na tisa kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali kunyesha usiku wa kuamkia leo katika maeneo tofauto mjini Shinyanga.
ITV imefika katiktika eneo la shule ya msingi viwandani iliyoko katika kata ya Ibadakuli mjini Shinyanga muda mfupi baada ya mvua hiyo kunyesha na kukuta vyumba vinne vya madarasa,ofisi ya walimu na vyoo vya wanafunzi vyote vikiwa vimeezuliwa paa na kusababisha uharibifu mkubwa wa vifaa vya kujifunzia ikiwemo vitabu na madaftari ya wanafunzi.
Mbali na shule hiyo kupata maafa na kusababisha wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo maeneo mengine yaliyoathirika na na mvua hiyo na kaya kadhaa kukosa mahali pa kujisitiri ni eneo la Kitangili,Ubweti na Kizumbi ambapo baadhi ya wahanga wa mvua hiyo wanaeleza tukio lilivyotokea.
Akithibitisha kwa njia ya simu kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amesema mbali na mvua hiyo kusababisha maafa hayo mvua hiyo imesababisha kukatika kwa umeme usiku kucha hali ambayo imesababisha ugumu wa kufuatilia tukia kufuatia maji kutapakaa na kiza kikali.
No comments