Mtoto adaiwa kukeketwa, afa

Mtoto adaiwa kukeketwa, afa

Arusha. Mtoto wa miaka mitatu, Nuru Loshipha maarufu Tumaini amefariki dunia kwa madai ya kukeketwa katika Kata ya Mwandeti ya Wilaya ya Arumeru mkoani hapa.

Mmoja wa wanafamilia ambaye hakutaka jina lake litajwe kutokana na tukio hilo kufanywa siri, alidai lilitokea Desemba 28, mwaka jana baada ya mtoto huyo kukeketwa na kutokwa damu nyingi.

“Baada ya wahusika kuona anatokwa damu nyingi huku akiishiwa nguvu, waliamua kwenda naye duka la dawa kupata matibabu ambako mhudumu aliwataka wampeleke hospitali na akiwa njiani alifariki,” alidai mwanafamilia huyo.

Mhudumu wa duka la dawa la Kidali alikofikishwa mtoto huyo, Jane Andrew alithibitisha kumuona lakini hakumpatia matibabu kutokana na hali yake kuwa mbaya.

Source: Mwananchi

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.