Mbunge Wa Tanga Awaokoa Askari Wa Jiji La Tanga Na Kipigo Kutoka Kwa Wasafirishaji
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mhina Mustapha Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na wasafirishaji wanaofanya shughuli zao kati ya Mombasa nchini Kenya kuhusu kuwataka kuhamia eneo la stendi mpya ya kange kwa ajili ya kutoa huduma zao kulia mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mhina Mustapha Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na wasafirishaji wanaofanya shughuli zao kati ya Mombasa nchini Kenya kuhusu kuwataka kuhamia eneo la stendi mpya ya kange kwa ajili ya kutoa huduma zao katikati mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga,Alhaj Mussa Mbaruku
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mhina Mustapha Selebosi akisisitiza jambo kwa wasafirishaji hao kulia kwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) alhaj Mussa Mbaruku jana amelazimika kuingilia kati na kuwaokoa askari wa Jiji la Tanga waliotaka kupigwa na wafanyabiashara wa magari yaendayo Mombasa nchini Kenya kwa madai ya kukamata magari yanayotakiwa kuhamia stendi ya kange na kuwatoza
faini bila ya kuwa na mashine za EFDs.
Askari wa Jiji la Tanga ambao walinusurika kipigo hicho na kumlazimu Mbunge huyo kuwaingilia kati na kuwaondoa eneo hilo ni Timime Makasi na Emanuel Lyimo ambao walikuwa tayari wamezingizwa na wafanyabiashara hao wakijiandaa kuwatembezea mkongoto.
Magari hayo yalikuwa yamepakiwa kwenye eneo la barabara 10 karibu na Assad Hotel ambapo kumekuwa kukipakiwa magari yanayoelekea Mombasa nchini Kenya ambapo askari hao walidaiwa kukamata moja ya gari linaloelekea mjini Mombasa na kulitaka kulitoza faini.
Baada ya kuwepo na kadhia hiyo ilimlazimu Mbunge huyo ambaye yupo mkoani Tanga mapumziko ya mwishoni mwa wiki kabla ya kwenda mkoani Dodoma kuendelea na vikao vya kamati aliamua kufika eneo la tukio na kuwachukua askari hao kwa gari lake na kuwapeleka mpaka kwenye ofisi zao zilizopo Kata ya Nguvumali Jijini Tanga.
Akizungumza na wasafirishaji hao,Mbunge huyo aliwataka kuwa watulivu kwani suala hilo linajadilika na huenda likapatiwa ufumbuzi kutokana na vikao vya baraza la madiwani ambavyo vinatarajiwa kuketi hivi karibuni mjini hapa.
Aidha pia Mbunge huyo alishtusha na kitendo cha askari hao kuchukua ushuru bila ya kutumia mfumo wa kieletroniki jambo ambalo ni kunyume na utaratibu wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.
Hata hivyo askari, Timime Makasi ambaye ni askari wa Jiji ambaye alisema wao wanafanya kazi chini ya Halmashauri ya Jiji hilo na wanatekeleza agizo hilo kama walivyoelekezwa ya kukamata gari zote ambazo zinatakiwa kupaki kwenye stendi kuu ya Kange.
Alisema kufuatia agizo hilo la halmashauri la kuzikamata gari hizo na atakae kwenda kinyume atatakiwa kutozwa faini ya shilingi 50,000 jambo lililozua utata baada ya askari hao kuonekana kutokuwa na mashine za kielektroniki.
Aidha pia mmoja wa wamiliki wa magari yanayofanya safari zake za Tanga Mombasa Mohammed Nassor alisema kuwa swala liliwashitua zaidi ni kutokuwepo na mashine hizo za risiti kama Serikali ilivyoelekeza jambo ambalo lilitaka kuzua mzozo baina ya wafanyabiashara na askari hao.
Akizungumzia sakata hilo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi alisema halmashauri ina uhaba wa mashine za EFDs na hawaruhusu askari hao wa Jiji kuchukua ushuru bila kuwepo kwa mashine hizo.
Alisema wanachotakiwa kukifanya askari hao ni kulikamata gari na kulipeleka depo ya Halmashauri ambao ndio kunafanyika taratibu za kutozwa faini kwa mfumo wa mashine za EFDs.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
No comments