Kiasi cha Fedha Serikali ilichopata Tangu Kuanza Mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amesema kuwa kwa kipindi cha kati ya mwezi Mei hadi mwezi Disemba mwaka jana, serikali ilifanikiwa kukusanya kiasi cha fedha TZS bilioni 19 katika mradi wa mabasi yaendayo haraka.

Hayo yamesemwa na Waziri Simbachawene leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku moja tangu Rais Dkt Magufuli alipomtaka waziri huyo kwa kushirikiana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa kueleza umma nikiasi gani wamekusanya ili ifahamike kama mradi huo unaingiza faida au ni hasara.

Waziri Simbachawene pia ameagiza vikosi vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinawaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga wanaofanya biashara zao ndani ya eneo la barabara hiyo kitu ambacho ni kinyume na sheria.

Aidha, wakati huo huo Waziri Simbachawene amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote nchini kuhakikisha wanawachukulia hatua za kisheria wazazi wote wanaotekeleza watoto wao au kuwatuma kwenda kuwa ombaomba jambo linalopelekea ongezeko la watoto wa mitaani.

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.