Je wajua Azam wameingia fainali bila kuruhusu hata bao moja Mapinduzi Cup?
Je wajua Azam wameingia fainali bila kuruhusu hata bao moja Mapinduzi Cup?
Na Abubakar Khatib ‘Kisandu’, Zanzibar.
Timu ya Azam FC imeweka rekodi kuwa timu pekee kufika fainali katika mashindano ya kombe la Mapinduzi 2017 bila kuruhusu kufungwa hata bao moja.
Azam wametinga fainali baada ya kuitoa Taifa ya Jang’ombe kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali ambapo katika makundi pia michezo yake yote mitatu hawakruhusu bao hata moja.
Walianza mchezo wao wa kwanza kwa kuifunga Zimamoto ya visiwani Zanzibar bao 1-0, wakatoka sare tasa (0-0) na Jamhuri ya Pemba kisha kuifuga Yanga kipigo kitakatifu cha mabao 4-0, hivyo imecheza michezo zote hizo bila ya lango lao linalolindwa na Aishi Manula kuguswa.
Ijumaa January 13, 2017 Azam FC watacheza fainali na timu ya Simba mchezo utakaopigwa majira ya Saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Hii ni fainali ya tatu kwa upande wa Azam katika mashindano hayo ambapo iliwahi kucheza mara mbili mfululizo mwaka 2012 na 2013 na zote walifanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuzifunga timu ya Jamhuri na timu ya Tusker ya Kenya, hivyo Azam inahistoria nzuri ya kutopoteza michezo ya fainali katika kombe hilo.
No comments