Fursa Za Kielimu Nchini Uturuki
Watanzania wamepewa changamoto ya kuchangamkia fursa za masomo zinazopatikana nchini Uturuki, ili waweze kujipatia taaluma bora katika fani mbalimbali na kutoa mchango unaohitajika katika maendeleo ya nchi.
Changamoto hiyo imetolewa na wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma elimu ya juu nchini Uturuki kwa ufadhili wa Serikali ya hiyo, ambayo hutoa nafasi za masomo kwa wanafunzi kutoka pande mbalimbali za ulimwengu ikiwemo Afrika na Asia.
Wanafunzi hao wamesema Uturuki ni taifa ambalo limepiga hatua kubwa kiuchumi na kimaendeleo na vyuo vyake vikuu vina sifa ya kutosha na vinaheshimika duniani kote.
Rais wa Uturuki bwana Recep Tayyip Erdogan anatarajiwa kuwasili nchini kesho akifuatana na ujumbe wa watu 200, ambapo pamoja na mambo mengine, ziara yake hiyo itahusu zaidi kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Uturuki katika nyanja za elimu na utamaduni.
No comments