FATA NYAYO ZA BILIONEA WA FACEBOOK UFANIKIWE
NIANZE kwa kukubaliana na wasomaji ambao wamekuwa wakilalamika kuyumba kiuchumi kwani hata mimi ninapitia kipindi kama hicho. Lakini cha msingi tusikate tamaa, tuendelee kukaza kwa kufanya kazi kwa bidii. Tusisahau ubunifu na kukipenda kile tunachokifanya ambacho mwisho wa siku ndicho kinatupatia mkate wetu wa siku. Baada ya kusema hayo, bila shaka utakuwa umewahi kutumia au kusikia Mitandao ya Kijamii ya Facebook, WhatsApp na Instagram.
Mmoja wa wamiliki wa mitandao hiyo anajulikana kwa jina la Mark Zuckeberg, Mmarekani aliyezaliwa huko White Plains, New York nchini Marekani. Jamaa ni bilionea mwenye pesa ndefu ambazo zimemfanya ashike namba tano huku akiwa na utajiri wa dola bilioni 55 (zaidi ya trilioni 110), ndiye tajiri mdogo zaidi akiwa na umri wa miaka 32.
Mkewe anaitwa Priscilla Chan mwenye umri wa miaka 30. Jamaa ametajirishwa na Mtandao wa Facebook. Hakuzaliwa akiwa tajiri, aliangalia dunia inahitaji nini, hivyo akachangamkia fursa. Ni mambo yaleyale ambayo nimekuwa nikiyaeleza kila siku. Alipoona fursa, hakuiacha, akaichangamkia na mpaka kufika hapo. Anapohojiwa na waandishi wa habari, huzungumza mambo mengi sana ambayo kama watu wengine wakiyafanya, basi watafanikiwa na kuwa kama yeye.
Unataka kufanikiwa? Basi fanya mambo haya matano ambayo yamemfanya Zuckerberg kufanikiwa na kuwa hapo alipo. USIOGOPE KUFA NYA MAKOSA Wakati akihojiwa kwenye vipindi mbalimbali vya televisheni Zuckeberg anasema: “Watu wengi wanaogopa kufanya mambo f’lani kwa kuogopa kukosea. Hakuna mtu aliyekamilika, kila mtu huanza kwa kufanya makosa pia. Wengine wanaogopa kuchekwa, eti nikikosea, akina f’lani watanicheka, ndugu yangu, hutakiwi kuogopa kitu chochote kwani kukosea ni sehemu ya maisha yetu, ni kitu ambacho tumeumbwa nacho.
“Unapofanya makosa ndipo unapopata akili ya kufanya vizuri baadaye na ndiyo maana wakati mwingine unapata utajiri, unafanya makosa na kufilisika lakini unaporekebisha makosa yako na kugundua ulipoangukia, unainuka tena.” JIFUNZE KWA WATU WALIOFANIKIWA Zuckerberg anaendelea: “Unapotaka kufanikiwa ni lazima uwaangalie waliofanikiwa walianzaje? Nilipoanza safari hii, niliwaangalia Bill Gates, Carlos Slim na wengine. Ni mfano bora kwangu. Niliangalia video zao na kuwasikiliza, kwa nini walifanikiwa, waliwezaje?
Kama wao waliweza, kwa nini mimi nishindwe? Nikafanya na hatimaye nikawa hapa nilipo.” T E N GENEZA T I M U NZURI J a m a a anafunguka: “Huwezi kufanya biashara ukiwa peke yako, ni lazima uandae timu kwa ajili ya usimamizi, sasa hiyo timu ni lazima iwe nzuri ambayo itakufanya kusonga mbele na si kurudi nyuma. “Nilipoanzisha Facebook, niliiandaa timu yangu, niliweka watu makini, timu ambayo ilikuwa tayari kupambana.
Walijitoa sana, walipambana na ninakiri kwamba bila timu hiyo makini leo nisingekuwa hapa nilipo.” UWE NA KIU YA MABADILIKO Anasema: “Ndiyo! Unapoamua kufanya biashara mtaani kwako, ni lazima uwe na kiu ya kubadilisha mtaa mzima. Watu wana shida na kitu f’lani waambie kwamba wewe utabadilisha kila kitu. Watu wanapenda mabadiliko, biashara ambayo inafanyika, leta yako ikiwa imeboreshwa au yako iwe mpya kabisa kwa ajili ya kuonesha watu kwamba
una kitu kipya kuliko vya w e n gine. “Niliangalia hilo kipindi cha nyuma.
Niliona kwamba watu wanapenda kuwasiliana, wale wa Marekani wanapenda kuwasiliana na marafiki wapya wa Afrika, Ulaya na sehemu nyingine. “Nilipogundua hilo, nikasema ni lazima nilete mabadiliko, watu watoke kwenye hali ya kutamani na kuingia kwenye hali ya kuwa nacho, hivyo nikawaletea Facebook ambayo leo watu wa sehemu mbalimbali wanatengeneza urafiki.
”FUATILIA KILA SIKU Jamaa anaweka wazi: “Unapokuwa na biashara usijifanye wewe ndiye bosi kwamba huwezi kutoka ofisini, unataka kila kitu uletewe. Haipo hivyo, kwa sasa hivi kila kitu kimebadilika, hakuna bosi wa kukaa ofisini, kama ni kweli hiyo ni biashara yako ni lazima uifuatilie hatua kwa hatua. “Huwezi kupata mafanikio kwa kukaa ofisini tu, ni lazima ujue leo kimeingia kiasi gani na kimetoka kiasi gani, ni lazima ujue timu yako inaishi vipi, f’lani yupo wapi na anafanya nini. Ni lazima wakati mwingine uende kuzungumza na watu, upate mawazo yao, hawataki nini na wanataka nini.
Ukifanya hivyo na kujitolea, hakika utazidi kufanikiwa.”
No comments