Fanya yafuatayo uongeze uwezo wa kufikiri

Ubongo ni sehemu ya ajabu sana katika mwili wa binadamu. Pia Ubongo ndio unatofautisha uwezo wa kufiliri kati ya mtu mmoja na mwingine.

Hizi ndizo njia zilizothibitishwa za kuuongeza uwezo ubongo wako. Ila kitu kubwa kwanza unatakiwa kuwa na nia.

1. Mazoezi Ya Mara kwa Mara
Mazoezi yana uwezo wa kuchangamsha chembe hai za ubongo kwa kupitia mfumo wa neva "neurogenesis". Pia mazoezi ya misuli husaidia katika kupunguza msongo wa mawazo. Ni njia ambayo ni rahisi na ni bure.

2. Fanya Mazoezi ya Ubongo
Hii inawezekana kwa kucheza michezo inayotumia akili kama "Draft" na michezo mingine ambayo pia hupatikana katika simu kama "Sudoku, Crosswords puzzles". Pia kuna mchezo kama dual-n-back. Michezo ya kutumia akili kuchangamsha na kuuamsha Ubongo. Mwaka 2008 wanasayansi Susanne Jaeggi and Martin Buschkuehl walisema kucheza michezo ya akili husaidia kuongeza "fluid intelligence".
            
3. Kusoma
Kusoma pia husaidia katika kufikiri, hii ni pale unaposoma  kitabu ambacho hukuwahi kusoma, pia kusoma magazeti. Lakini unapaswa kujua kusoma kitabu ambacho ni kirahisi sana hakikusaidii chochote bali kukufurahisha tu. Kuwaasa watoto wadogo kujisomea na kusoma vitabu hii itawaongezea uwezo wao wa kufikiri. Mfano unahitajika kusoma riwaya (novel) ambazo zitakufanya ufukirie kitu au baadhi hata misamiati ikufanya utafute kamusi (Dictionary).

4. Usije Ukaacha kujifunza
Kutokufikia mwisho kujifunza kitu husaidia katika kufikiri, hii ni pale unaposoma  kitabu ambacho hukuwahi kusoma, pia kusoma magazeti. Lakini unapaswa kujua kusoma kitabu ambacho ni kirahisi sana hakikusaidii chochote bali kukufurahisha tu. Kuwaasa watoto wadogo kujisome na kusoma vitabu hii itawaongezea uwezo wao wa kufikiri. Mfano unahitajika kusoma riwaya (novel) ambacho zitakufanya ufukirie kitu.

5. Fanya Tafakari ( Meditation)
Meditation ni kitendo cha kufundisha ubongo kukumbuka na kutafakari. Pia Kufanya tafakari  husaidia kuongeza uwezo wa damu kuzunguka vizuri katika ubongo. Fanya tafakari angalau dakika 30 kwa siku ila sio lazima iwe kwa mara moja inawezekana ukaigawanya kwa dakika kumi kumi mara tatu  kwa siku. Ila unashauriwa pale unapoamka ndo ufanya tafakari.

6. Kula Vizuri
Kuwa makini katika ulaji wa chakula kuna baadhi ya vyakula ni kwa ajili ya kujaza tumbo "Junk food" ila mojawapo ya vyakula unavyohitajika kula ni pamoja na samaki angalau mara tatu kwa wiki, nyama, watafiti wanasema chai (kwa asubuhi) ni chakula cha ubongo, Vitamini B na E, Parachichi (Avocado)Pia epuka chakula cha mafuta mengi.

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.