AFCON 2017: UGANDA VS GHANA


 Mlinda mlango wa Uganda Dennis Onyango ndiye mchezaji bora wa Afrika kwa ligi za ndani

Kocha wa Ghana Avram Grant amesema anataka kufika mbali zaidi katika fainali za mwaka huu tofauti na ilivyokuwa mwaka 2015 walipofungwa na Ivory Coast kwa njia ya penalti.

Mshambuliaji Asamoah Gyan na kiungo wa West Ham Andre Ayew walikuwa miongoni mwao miaka miwili iliyopita na uzoefu wao unatarajiwa kuwasaidia katika mchezo wa leo.

Wachezaji wa Uganda Murushid Juuko na Khalid Aucho wote hawatakuwepo katika mchezo huo.

Milutin 'Micho' Sredojevic amefundisha nchi sita tofauti za Afrika tokea mwaka 2001

Cranes wanaingia katika michuano hiyo tokea mwaka 1978 walipopoteza dhidi ya Ghana katika hatua ya fainali, lakini wakati huu wanaingia wakiwa ndio timu bora ya Afrika 2016.

Katika mchezo wa mwisho kwa timu hizi kukutana zilitoka suluhu ya 0-0 na hapa ilikuwa kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 nchini Urusi.

Ghana nao wanataka kushinda kombe hili ambalo hawajalipata tokea mwaka 1982.

 Mara ya mwisho Ghana kushinda kombe hili ilikuwa 1982

Mafanikio makubwa kwa Uganda katika michuano hii ni ushindi wa pili miaka 39 iliyopita.

Ghana ni ya nane barani Afrika na ya 54 duniani wakati Uganda inashika nafasi ya 18 Afrika ya ya 73 duniani.

Michezo ya kundio D itapigwa katika uwanja wa Stade de Port-Gentil

Mchezo huu utatangazwa moja kwa moja na idhaa ya kiswahili ya BBC saa 6:30 saa za Afrika Mashariki.

No comments

Content by MwasebaINFO.All RIghts Reserved. Powered by Blogger.